Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Mfano
Katika kumwabudu Mungu mwili wote unaabudu. Akili, mwili na roho ni vifaa muhimu katika ibada. Vyote vinategemeana. Wakorintho walithamini sana kunena kwa lugha. Hawakuelewa kuwa karama hii siyo chombo cha kufanya uinjilisti miongoni mwa wasiomjua Kristo. Kwa hawa kunena kwa lugha ni isharaya hukumuinayowathibitishia kutoamini kwao, maana wanaona wanenaji wana wazimu. Lakini wasiomjua Kristo wakihutubiwa Injili kwa lugha wanayoelewa, yawezekana kuwaleta kwa Kristo ili wamwamini.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz