Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 19 YA 31

Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo (m.18). Kwa maneno haya Yohana Mbatizaji alikuwa amekemea dhambi ya Mfalme Herode. Ilikuwa ni hatari kubwa, lakini Yohana alimwogopa Mungu kuliko wanadamu. Na kweli, Mfalme Herode alikasirika, akamfunga Yohana gerezani. Mwisho Yohana akauawa, ila Herode mwenyewe hakupenda iwe hivyo, maana Herode alimwogopa Yohana; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu (m.20). Fundisho ni kwamba sifa nzuri ya mtumishi wa Bwana ina nguvu kubwa katika jamii (ling. Mt 5:16 ambapo Yesu anasema, Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni)!

siku 18siku 20

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana