Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 20 YA 31

Yesu aliona tatizo ambalo tunaliona pia leo katika kanisa, hasa kwa wachungaji, wainjilisti na wahudumu wengine: Kwa upande mmoja kazi ni nyingi. Watu wanahitaji sana huduma! Wakampa habari za mambo yote waliyoyafanya, na mambo yote waliyoyafundisha (m.30). Akaona mkutano mkuu, akawahurumia ... akaanza kuwafundisha mambo mengi (m.34). Kwa upande mwingine ni lazima kupata nafasi ya kupumzika na kula! Njoni ninyi peke yenu kwa faragha ... mkapumzike kidogo (m.31). Wakala wote wakashiba (m.42). Tafakari kama kuna uwiano wa kufanya kazi na kupumzika katika maisha yako!

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana