Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 2 YA 31

Akabatizwa na Yohana katika Yordani (m.9). Yohana alikuwa amehubiri kuwa Yesu ni mkuu kuliko yeye (m.7-8, Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake. Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu). Kama ni hivi, kwa nini Yesu abatizwe na yeye? Jibu linapatikana katika Mt 3:14-15, pale Yohana alipotaka kumzuia Yesu, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi [Yohana] akamkubali. Ubatizo wa Yohana ulikuwa ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi (m.4). Ila Yesu hakuungama dhambi zake binafsi bali dhambi zetu, dhambi za ulimwengu wote. Ushahidi wa Yohana baada ya Yesu kubatizwa ni huu: Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Yn 1:29). Hii ni Injili, ni habari njema kweli! Na utayari wake Yesu ulimpendeza sana Mungu, maana mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake; na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe (m.10-11). Zingatia wito wa Yesu katika m.15: Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.

Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz