Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano
Yesu aliwasaidia watu kiroho na kimwili. Kiroho aliwasaidia kwa kufundisha na kuihubiri Habari Njema (m.21-22, Mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha. Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi. M.39, Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya). Kimwili Yesu aliwasaidia kwa kuponya magonjwa yao. Walikuwa wakimletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo (m.32). Ni muhimu sana sisi Wakristo kuzingatia kuwa Yesu alitofautisha kati ya wagonjwa wa kawaida na wenye pepo! 1. Alimponya mtu mwenye pepo kwa kumkemea pepo (m.23-27). 2. Alimponya mtu mwenye homa ya kawaida (m.29-31). Tusiwatie watu hofu ya kuwa na pepo kama hawana!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz