Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

SIKU 18 YA 31

Abishai alikuwa ni mdogo wake Yoabu, mkuu wa jeshi. Mama yao aitwaye Seruya alikuwa ni dada yake Daudi. Wote ni washupavu. Uhusiano kati yao na Daudi ulikuwa wa kipekee. Kwa upande mmoja walikuwa waaminifu sana kwa mfalme! Kwa upande mwingine walikuwa ni wabishi. Mara chache ilitokea kwamba hawakumtii Daudi; waliona uamuzi wao ulifaa zaidi. Mara nyingi walikuwa na haki! Ila kukosa utii kulimfanya Daudi kuwaona kama adui zake; hasa kutokana na tendo la kumwua Absalomu. Lakini 19:21-22 inaonyesha kwamba pia maoni yao mengine yalisababisha hiyo: Abishai, mwana wa Seruya, akajibu na kusema, Je! Shimei hatauawa kwa sababu hii, kwa kuwa amemlaani masihi wa BWANA? Lakini Daudi akasema, Mimi nina nini nanyi, enyi wana wa Seruya, hata mmekuwa adui zangu leo? Je! Atauawa mtu ye yote leo katika Israeli? Kwa maana sijui mimi leo ya kwamba ndimi mfalme juu ya Israeli?

siku 17siku 19

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021

Soma Biblia Kila Siku Oktoba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa oktoba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu utasoma zaidi Zaburi, 2 Samweli na Ufunuo. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/