Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Mungu anapoadhibu watu wake, inayotakiwa kufanyika ni toba kama ile katika m.18a:Bwana ndiye mwenye haki; Maana nimeiasi amri yake; Sikieni, nawasihi, enyi watu wote, Mkayatazame majonzi yangu. Tunaona mji wa Yerusalemu unajua kuwa Mungu ameuhukumu kwa haki kwa sababu ya dhambi zake. Haupati huruma unayoililia, maana tukimwacha Mungu hakuna mfariji tena. Tuzingatie watu wanavyoonywa wajifunze kutokana na hali ya Yerusalemu. Uhalifu wake umetokeza madhara makubwa kwa wakazi na mali. Yerusalemu unasema:Naliwaita hao walionipenda Lakini walinidanganya; Makuhani wangu na wazee wangu Walifariki mjini; Hapo walipokuwa wakitafuta chakula ili kuzihuisha nafsi zao. Angalia, Ee Bwana; maana mimi ni katika dhiki; Mtima wangu umetaabika; Moyo wangu umegeuka ndani yangu; Maana nimeasi vibaya sana; Huko nje upanga hufisha watu; Nyumbani mna kama mauti(m.19-20). Tuwe na busara. Tujifunze kutokana na yawapatayo wengine, tusisubiri hadi yatukute sisi wenyewe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/