Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

SIKU 31 YA 31

Je, unafanana na nani utoapo? Tusimpe Bwana katika mali iliyotuzidi tu, bali tukubali hata kupunguza starehe yetu ili kazi ya Bwana itendeke! Hata katika utoaji wetu ufalme wa Bwana uwe jambo la kwanza, kama Yesu anavyosema katikaMt 6:33,Utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Kuanzia m.5 tuna hotuba ya Yesu kuhusu mambo yatakayotokea baadaye hapa duniani. Swali la wanafunzi kuhusu kubomolewa kwa hekalu (m.5-7) anajibu kipekee katika m.20-24.Jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Ila hotuba yake yahusu zaidi mambo yatakayotokea siku za mbele zaidi. Ina maonyo (m.8-9, Msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba), na faraja (m.14-15 na 18-19,Mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. ...Baba yako aonaye sirini atakujazi)!

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/