Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano
Vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu(m.25). Kwa neno hili fupi Yesu ametupa mwongozo wa msingi namna ya kuishi kama Mkristo katika ulimwengu huu. Yesu anataka tuitii serikali kwa sheria zake, hata kama twaona si haki. Maana serikali haiwezi kuwa na mamlaka bila kibali cha Mungu (kama una nafasi tafuta kusoma Rum 13:1-7). Lakini pia Yesu anataka tumtii Mungu kwa sheria zake. Katika suala la pesa, tutoe kwa hiari tunayodaiwa na serikali na vilevile tunayodaiwa na kanisa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/