Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

SIKU 22 YA 31

Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea (m.10). Yathibitisha kwamba kila binadamu ana thamani kubwa kwa Mungu. Bila shaka hata katika jamii yetu tunapokaa sisi kuna watu wanaohesabiwa kuwa wabaya kama vile huyo Zakayo alivyohesabiwa katika jamii ile. Unaonaje kwenda kumtembelea mtu mbaya ili kumshuhudia habari za Yesu? Je, unafanana na watu hawa waliotajwa katika m.7?Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Yesu hakusita alipoona Zakayo ana hamu ya kumwona. Zakayo alimpokea nyumbani mwake na hata moyoni mwake. Aliokoka na maisha yake yalibadilika mara.Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu(m.8-9).

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022

Soma Biblia Kila Siku Machi/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Maombolezo na Luka. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/