Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarijio / Sehemu ya 2 - Matendo ya MitumeMfano

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

SIKU 17 YA 20

Paulo anasimama mbele ya baraza la viongozi wa dini ili kujitetea. Baada ya kukatizwa kwa fujo na kufikiria kimakosa kuwa kuhani mkuu alikuwa mtu mwingine, Paulo anaona kuwa hali si nzuri na anajaribu kufikiria cha kufanya. Anaona kuwa baraza limegawanyika kwa madhehebu mawili ya kidini: Masadukayo na Mafarisayo. Masadukayo hawaamini uhalisia wa ufufuo au malaika, huku Mafarisayo wakifasiri sheria kwa shuruti zaidi na wanaamini katika uhalisia wa kiroho unaokataliwa na Masadukayo. Paulo anaona mgawanyiko huu kati ya baraza kama fursa ya kuondoa umakinifu kwake, na anaanza kupiga kelele kuwa yeye ni Mfarisayo na ameshtakiwa kwa tumaini la ufufuo wa waliokufa.

Kutokana na hili, mjadala mrefu unaanza.Iinaonekana Paulo anafanikiwa kwa haraka, na hata Mafarisayo wanaanza kumtetea Paulo. Lakini baada ya muda mfupi, ubishi unakuwa mkali hadi maisha ya Paulo yanakuwa hatarini tena. Anaondolewa kutoka kwa vurugu zilizojitokeza na kamanda wa Kirumi, na kuwekwa kuzuizini kinyume na sheria. Usiku unaofuata, Yesu aliyefufuka anasimama kando ya Paulo ili kumtia moyo, akisema kuwa kwa kweli Paulo atatekeleza kusudi la Yesu ndani ya Rumi. Kwa hivyo asubuhi, wakati dada wa Paulo anapomtembelea ili kumwambia kuwa zaidi ya Wayahudi 40 wanapanga njama ya kumvamia na kumuua, Paulo ana neno kuu la faraja linalompa msingi wa kusimamia. Uvamizi hautafaulu kukwamisha huduma ya Paulo. Ataishi na kuiona Rumi, kama tu Yesu alivyosema angeiona. Kama ilivyotarajiwa, onyo linamfikia kamanda kwa muda ili kukatiza njama hiyo. Paulo anapelekwa Kaisaria na zaidi ya wanaume 400 waliofunzwa ili kuhakikisha kuwa anawasili salama.

Soma, Tafakari, kisha Ujibu:

• Wakati mwingine Yesu huwaondoa watu wake katika matatizo, na wakati mwingine anakutana nao katikati yake. Paulo aliona uwepo wa Yesu kwa njia ya kipekee katika jaribio lake la kipekee. Lakini wafuasi wote wa Yesu, iwe wanauona au kuuhisi au la, wana ahadi ya kila siku, kuwa Yesu yuko nao na hawezi kuwaacha (Mathayo 28:20). Mawazo gani na hisia zipi zinaibuka unavyofikiri kuhusu hili?

• Chukua nafasi na uombe. Dhihirisha imani yako na shukrani kwa Yesu. Ongea na Mungu kuhusu mambo ambayo ni mazito kwa moyo wako. Muombe akusaidie kuona na kuuishi uwepo wake katikati ya hali ngumu unazopitia.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Ufalme Unaoenda  Kinyume na Matarijio  / Sehemu ya 2 - Matendo ya Mitume

BibleProject ilibuni Ufalme Unaoenda Kinyume na Matarajio Sehemu ya 2 ili kuwatia watu moyo, vikundi vidogo, na familia mbali mbali waweze kusoma Matendo ya Mitume kwa siku 20. Mpango huu unajumuisha video za katuni, mihtasari yenye mawazo yanayojenga, na maswali ya tafakari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu na kuzama kwenye ubunifu wa fasihi wa mwandishi na kuelewa na kujifunza kutoka kwenye mtiririko wa mawazo yake.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com