Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
![Soma Biblia Kila Siku Juni/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F31560%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kumfurahia Mungu kwa kweli ni pale tunapohesabu baraka zake katika yale yote anayotutendea, makubwa na madogo. Yatupasa kumshukuru Mungu na kuyafurahia mambo hayo. Hivi ndivyo Paulo alivyoishi na anatutaka tuige kwake. Hata alipopungukiwa, aliyahesabu hata hayo kuwa mapenzi mema ya Mungu kwake. Mioyo inayompokea Mungu hivyo huruzukiwa amani ya kweli, hata kama kuna kupungukiwa na mahitaji ya kimwili. Kwa njia hii, twaweza kuona tukiyaweza yote kwa sababu Mungu ndiye mdhibiti.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku Juni/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F31560%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/