Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano
![Soma Biblia Kila Siku Juni/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F31560%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kanisa la Filipi halikuwa na utajiri wa mali nyingi, lakini lilikuwa hodari kumtolea Mungu sadaka zilizotumika kutunza kazi ya Injili. Walichangia wahitaji nje ya Ugiriki na Paulo anasema hili litawawia baraka. Twaona katika 2 Kor 8:1-4 kwamba walijitoa kwa kiwango kilichozidi hata uwezo wao:Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia, maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia wakatatifu. Kumtolea Mungu namna hii ni kuzuri na twapaswa kuiga kwa ndugu hawa. Lakini ni muhimu kukumbuka kujitoa kwanza nafsi kwa Bwana kama ambavyo wakristo wa Makedoniwalijitoa nafsi zao kwa Bwana(2 Kor 8:5). Kwa hiyo ni muhimu kumwamini Mungu na kuishi sawa na mapenzi yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku Juni/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F31560%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/