Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

SIKU 25 YA 30

Hali ya Yusufu ikawa tena ngumu. Lakini badala ya kumlaani Mungu akazidi kumtumaini.Bwana akawa pamoja na Yusufu. Maneno haya yameandikwa mara 4 katika sura hii (m.2, 3, 21 na 23)! Na bila shaka haya yaliandikwa kutokana na masimulizi aliyosimulia Yusufu baadaye. Yaani, Yusufu aliposimulia habari hizi kwa ndugu zake na watoto wake hakujisifu bali alimpa Bwana utukufu kwa kuwa Mungualimfadhili, akampa kibali machoni pa mkuu wa gereza(m.21)! Je, unaposimulia habari ya maisha yako kwa watoto wako unampa Mungu utukufu?

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/