Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

SIKU 29 YA 30

Nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri. Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani(m.15-16). Farao hakumtaja Mungu, ila alimpa Yusufu sifa yote. Hapo Yusufu alijaribiwa. Angeweza kujivuna akijipatia sifa mbele ya watu. Lakini alimpa Mungu utukufu moja kwa moja:Si mimi; Mungu atampa Farao. Huu ni mfano mzuri wa unyenyekevu! Je, wewe ulimpa Mungu utukufu pale alipofanikisha utumishi wako? Zingatia Neno la Mungu katika 1 Pet 4:10-11 linaposema,Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022

Soma Biblia Kila Siku Juni/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Juni pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wafilipi na Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabblia.or.tz/