Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

BibleProject | Hekima ya MithaliMfano

BibleProject | Hekima ya Mithali

SIKU 21 YA 32

Sura ya 20: Wenye Busara Huwa Waangalifu kwa Maneno yao

Katika sura hii tunapata tena mithali nyingi zinazotumia jina la agano la kibinafsi la Mungu, Yahweh. Pia kuna mithali nyingi zinazorejelea mfalme wa Israeli (mstari wa 2, 8, 26, 28). Hivyo katika sura hii, tunapata maudhui mazito kuhusu mamlaka ya kiungu, haki na hekima ya Mungu. Hekima huwa hupendeza zaidi unapotambua kuwa uko chini ya uangalizi wa Mungu na mfalme.

Sura hii inaangazia kuonyesha hekima kupitia maneno yetu. Tunaona kuwa maneno ya haraka, maneno matupu na maneno makali huwa na athari kubwa. Hivyo, kuwa mwangalifu katika unachosema. Unaposoma sura hii, angalia kwa makini mstari wa 6, 9, 11, 14, 19, 20, 22 na 25. Jiulize maneno unayonena yataonekana vipi mbele za Mungu na mbele za wanaokuongoza.

Mwisho, je, umetambua kwamba kadri tunavyozidi kuchambua misemo ya Sulemani, ndivyo hekima inazidi kuwa changamani? Misemo hii husomeka kama mafumbo— maana yake imejificha. Unapaswa kuchambua na kuwaza kuhusu kinachosemwa na kuhusu maneno yaliyotumiwa. Tenga muda usome sura ya 20 kwa undani zaidi ili ufahamu hekima inayozungumziwa.

Andiko

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

BibleProject | Hekima ya Mithali

Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.

More

Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili