BibleProject | Hekima ya MithaliMfano
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Sura ya 21: Pata Kinachokujia
Sura hii ina muundo wa kuvutia. Neno "Bwana" linajitokeza katika mistari ya kwanza 3 na mistari 2 ya mwisho, kama vile kauli tangulizi na tamatishi katika fasihi. Mada ya haki imewekwa katikati ya sehemu hizi mbili. Mpangilio huu maalum unatukumbusha kwamba Mungu ndiye mwanzo na mwisho— uovu unaweza kufanya mabaya yake, lakini haki itashinda.
Mstari wa 9 na 19 inazungumzia kuhusu mke ambaye ni mgumu kuishi naye. Mwanzoni inaonekana haina mpangilio maalum na haihusiani, lakini tunapoilinganisha na maudhui mengine makuu kwenye sura hii, inatekeleza jukumu la kimuundo. Mistari hii inagawanya sura katika sehemu 3 (mstari wa 4-10, 10-18 20-29).
Bruce Waltke, katika ufafanuzi wake kuhusu Mithali, anaainisha sura kwa njia hii:
•Mstari wa 1-3 Hekima Kuu ya Bwana
•Mstari wa 4-8 Kushindwa kwa waovu
•Mstari wa 9 Mke mgumu
•Mstari wa 10-18 Ushindi wa wenye haki dhidi yao
•Mstari wa 19 Mke mgumu
•Mstari wa 20-29 Furaha ya kudumu ya wenye haki
•Mstari wa 30-31 Hekima Kuu ya Bwana
Wazo kuu ni kuwa waovu watapata adhabu, lakini kama mstari wa 15 unavyotukumbusha, "haki inapotekelezwa, ni furaha kwa wenye haki." Haki ya Mungu ni jambo nzuri, lakini pia hutuliza na inapaswa kututia motisha kutafuta imani na hekima.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![BibleProject | Hekima ya Mithali](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F32818%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Kitabu cha Mithali kinasema kuwa hekima ya Mungu imedhihirishwa kupitia ulimwengu na unaalikwa kushiriki. Je, ni lipi chaguo la busara kuhusiana na pesa, kazi, uhusiano na shughuli za kimaisha za kila siku? Mwongozo huu wa siku 32 utakuwezesha kusoma kitabu cha Mithali hatua kwa hatua na kufahamu mwelekeo unaopaswa kuchukua.
More
Tungependa kushukuru shirika la BibleProject kwa kutoa mwongozo huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.bibleproject.com/swahili