Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Leo twasoma jinsi Yuda alivyomsihi Yusufu kwamba Benyamini asibaki Misri. Kwa kweli twaona Yuda ni fundi wa kusema kwa niaba ya ndugu zake. Tena ni wazi kwamba maneno yalitoka moyoni mwake, maana mwisho akafunga kwa tamko hili: Basi, sasa nakusihi, uniache mimi mtumwa wako nikae badala ya huyu kijana kuwa mtumwa wa bwana wangu; na huyu kijana umwache aende pamoja na nduguze (m.33). Yanafanana na maneno aliyotamka Simba wa Yuda, ambaye ni Yesu, aliposema, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila ya Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na zile muhuri zake saba. … Mwana-Kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote (Ufu 5:5-6). Unaweza pia kufikiri juu ya Yesu anavyosema katika Mk 10:45, Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Na katika Yn 18:8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/