Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022Mfano
Twasoma jinsi Yusufu alivyowapa ndugu zake jaribio la mwisho. Alitaka kuhakikisha kwamba kweli wamebadilika katika roho zao. Je, wangekuwa tayari kumwacha Benyamini Misri kama walivyomwuza yeye kwenda Misri huko nyuma? Katika m.16-17 Yuda anaonyesha mashaka na kwa masikitiko anasema, Tumwambie nini bwana wangu? Tusemeje! Tujivutieje haki? Mungu ameona uovu wa watumwa wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, sisi na yeye ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake. [Lakini Yusufu] akasema, Hasha! Nisifanye hivi; mtu ambaye kikombe kilionekana mkononi mwake, ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Nanyi enendeni zenu kwa amani kwa baba yenu. Ni kama vile Yusufu aliwapepeta ndugu zake ili kuona hawa ni kama makapi tu au ni mbegu zinazofaa. Linganisha hali hii na Zab 1:4-6 inayosema, Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo. Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. Linganisha pia na Yesu jinsi alivyomhoji Petro alipokutana naye tena baada ya ufufuo. Hapo alimwuliza mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? (Yn 21:15-17)
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Novemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/