Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 11 YA 31

Watu walimwona Yohana kuwa mtu mkubwa, lakini hakujivuna. Uaminifu na unyenyevu wa Yohana ulitokana na yeye kujawa na kumtukuza Yesu. Akijihesabu kuwa hastahili hata kuwa mtumwa wa Yesu (ni maana ya neno la mfano katika m.27, Mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kitatu chake). Tena aliona heshima yake mwenyewe ni kumshuhudia Yesu kwa watu wote. Alimtambulisha kuwa ndiye Kristo aliyetumwa na Mungu kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi ya ulimwengu. Hakika ndivyo alivyo Bwana Yesu. Alizichukua dhambi zote za ulimwengu. Tukimtazama yeye hata kumwamini, tunao uzima wa milele.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana