Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 10 YA 31

Yohana alitumwa mahususi na Mungu kumshuhudia Mwana pekee wa Mungu, Yesu Kristo, aliye nuru halisi amtiaye nuru kila mtu ulimwenguni (m.9). Lakini jambo la ajabu ni kwamba huyu Kristo, Mwana wa Mungu, hata alipokuwa katika ulimwengu aliouumba mwenyewe, ulimwengu haukumtambua wala watu walio wake hawakumpokea (m.10-11). Je, wewe unamtambua na kumpokea huyu Neno? Na unapenda kufanyika mwana wa Mungu? Ni kwa kumwamini Yesu tu, ndipo tunafanyika kuwa wana wa Mungu. Kwa maana wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake (m.12).

Andiko

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana