Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 9 YA 31

Neno tuliyesoma habari zake ni wa ajabu! Alikuwako tangu mwanzo pamoja na Mungu, maana ni Mungu. Vitu vyote vilivyoumbwa viliumbwa kupitia kwake. Pasipo Neno kisingeumbwa chochote kilichoumbwa (m.3, Pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika). Hebu fikiri pia ulimwengu ukiwa giza tupu! Maisha hayawezekani. Lakini sasa kwa sababu Neno ni nuru ya ulimwengu, maisha na uzima tele vyawezekana na kupatikana kwake. Je, huyu Neno ni nani hasa? Tafakari ilivyoandikwa katika Yn 1:14 pamoja na ushuhuda wa Yohana alipomwona Neno, Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli. Mshike sana huyu Neno na Nuru ya ulimwengu upate uzima tele ulio ndani yake.

Andiko

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana