Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

SIKU 8 YA 31

Mamajusi walikuwa watu wa Mataifa. Walifika Bethlehemu baada ya Yesu kuzaliwa, wakiongozwa na nyota toka mashariki. Waliifuata ili kuthibitisha kuzaliwa kwa mfalme (m.2). Habari hizi zilimtisha Mfalme Herode. Akawatuma waende kumwona mtoto, kisha warudi kumjulisha mahali alipo Yesu. Walifurahi kumwona mtoto, wakamsujudia na kumpa zawadi, kisha wakaondoka pasipo kurudi kwa Herode. Huu ni ujumbe muhimu katika majira ya ufunuo. Tumpokee Yesu kwa furaha, kwani yeye ni nuru ya ulimwengu, kama unabii wa Isaya unavyoahidi, Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru kuu; wale waliokaa katika nchi ya uvuli wa mauti, nuru imewaangaza (Isa 9:2).

Andiko

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku JANUARI/2023

Soma Biblia Kila Siku Januari/2023 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mithali, Yohana na Malaki. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana