Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

TumainiMfano

Tumaini

SIKU 2 YA 3

Wakati mwingine kumfuata Yesu kwaweza kukupeleka moja kwa moja katikati mwa dhoruba – ndani mwa moyo wa kutokuwa na tumaini. Hili ndilo liliwapata wanafunzi wa Yesu kwenye bahari ya Galilaya. Wao walikuwa wanafanya walichoambiwa wafanye, nao wakaingia katika usiku mbaya sana katika maisha yao. Twasoma, “Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo…” (Mathayo 14:22).

Ulielewa hilo? Yesu aliwalazimisha waingie chomboni. Wanafunzi walikuwa wakitii. Walikuwa wakisoma Bibliazao, wakilisikiliza Neno, na kufanya kilichosema. Lakini ikafanyika. Upepo ukaanza kupiga chombo chao ikitishia kuwaharibu. Maandiko yasema, “Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi…” (Mathayo 14:24).

Umewahi jihisi umepigwa pigo na kutaabika katikati ya kufanya kile haswa unaamini kwamba Mungu alikwambia ufanye? Najua, nimekuwa hapo. Natamani ningelikwambia kwamba kumfuata Yesu inamaanisha hutawahi kabili dhoruba zozote. Natamani ningekwambia kwamba yamaanisha maji ya maisha haya daima yatakuwa matulivu. Lakini siwezi kwa sababu Bibliayasema tofauti. Biblia ina hadithi nyingi kuwahusu watu waliokabili wakati mgumu walipokuwa wakifanya kile ambacho Mungu hasa aliwambia wafanye.

Wafuasi ni mfano mmoja. Waisraeli ni mfano mwingine. Waisraeli walipofikia bahari ya Shamu, Farao na jeshi lake walikuwa nyuma yao. Maji ya bahari nayo ilitanda kwa maili nyingi mbele yao.Hawakuwa na mahali pa kwenda japo walikuwa wamekwenda mahali hasa, Mungu alikowatuma.

Waligundua, kama vile wengi wetu tumegundua, ya kwamba, waweza kuwa katikati mwa mapenzi ya Mungu, nawe uwe umekwama katikati mwa kile kinacho onekena kuwa hali isiyokuwa na tumaini. Hii ikiwa jinsi hii, sitaki kamwe uchanganye majaribu au kutokuwa na tumaini na kutokuwepo kwa uwepo wa Mungu, au mipango yake. Yeye anakusudi na dhoruba zote anazoruhusu katika maisha yetu.

Kuna mahubiri mengi leo hii kama vile vilivyo vitabu vingi vya Kikristo vinayokuambia kwamba, ikiwa utamfuata Yesu, hutawahi kabili changamoto za maisha. Lakini hiyo haikuwa kweli kwa Yesu au awaye yote aliyemfuata. Hii ni kwa sababu Mungu wakati mwingine anaruhusu majaribu maishani mwetu kusudi ajidhihirishe kwetu kwa njia ambayo vinginevyo, tusingelimjua. Lakini, tufaidi au tusifaidi kutoka kwenye majaribu haya, au yatushinde inategemea zaidi jinsi twayaona na jinsi twamjibia Mungu katikati mwayo.

Kuwa katika majaribu si jambo la kufurahia. Lakini hauhitaji kuyapitia peke yako. Uchumi kuzorota kwaweza kuweka shinikizo kwenye fedha zako. Labda umepoteza kazi ila si kwa kosa lako. Au huenda shinikizo zilizoko zimeongezea hali mvutano pale nyumbani katika familia yako na sasa unakabili dhoruba katika ndoa yako au na watoto wako.

Popote dhoruba yako yaweza kuwa, haupo peke yako. Yesu yu pamoja nawe naye atakuhifadhi. Tega sikio, sikiliza sauti yake. Mtazame Yeye. Kumbuka, ikiwa maisha yatakufanya ujihisi kana kwamba unazama, mlinzi wa maisha yako hutembea juu ya maji.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Tumaini

Kutokuwa na tumaini ni tauni inayokabili watu wengi wakati moja au mwingine. Hali hii haijahifadhiwa kwa wachache waliochaguliwa. Hata wengi wa mashujaa wetu wa Biblia wanaoheshimika, waliteseka kutokana na kutokuwa na tumaini katika miida fulani fulani. Tony Evans anashiriki mawazo yake jinsi ya kuwa na tumaini, na kushinda hali hiyo ya kukata tamaa katika mpango huu mfupi wa kusoma.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/