Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

TumainiMfano

Tumaini

SIKU 3 YA 3

Tumaini laweza kukuendesha kwa mwendo mrefu. Kila mara ninapomshauri mtu yeyote ambaye anangangana na ngome za kimihemko, daima mimi huangalia kipimo chake cha tumaini. Kwa sababu unapokuwa umepoteza tumaini, utakuwa umepoteza kila kitu. Fafanuzi ya urahisi, tumaini ni imani kwamba kesho yangu itakuwa nzuri kuliko leo yangu. Daudi alijua kuhusu nguvu ya tumaini wakati ambapo maisha yalionekana kuwa hayana tumaini.

Zaburi 42:1 yasema, “Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji, vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.” Pasipo kusoma zaidi kwenye Zaburi, yaonekana kana kwamba kila kitu ni shwari kwa Daudi. Lakini sivyo. Aya ya tatu yasema hivi, “Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku…” Rafiki, machozi yako yanapokuwa chakula chako mchana na usiku, ina maana kwamba unateseka kwa kutokuwa na tumaini na kuvunjika moyo. Daudi anapoandika Zaburi hii, alikuwa ameshushika na nafsi yake kuvunjika moyo. Lakini bado hapa asema, atamkumbuka Bwana.

“Bwana ataagiza fadhili zake,” Daudi aandika (Aya 8). Japo Mungu hajafanya bado, Daudi kwa ujasiri anasema kwamba atafanya. Kwa hivyo anajinenea. Anajiandikia- anaadika jarida kwake mwenyewe kuhusu imani yake katika Mungu. Kuna wakati ambapo maisha huporomoka pande zote kwako, yawezekana rafiki zako huenda wasiwe karibu, au hata wanaweza kukwambia vitu visivyo sawa. Itakubidi uchukue jukumu la kuzungumza na nafsi yako mwenyewe. Jitazame katika kioo na unene kweli ya Mungu. Jiandikie maneno kwenye vijikaratasi kisha uache mahali ambapo unaweza kuziona. Jipe moyo. Hivi ndivyo Daudi alivyofanya mara kadhaa.

Anajiuliza, “Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu?” Hakani uchungu wake wala kuukwepa, badili yake anaukabili na kuijiambia mwenyewe anachostahili kufanya. “Umtumaini Mungu; kwa maana nitakuja kumsifu, aliye afya ya uso wangu, na Mungu wangu. (Aya 11).

Kilichobadilisha hisia za Daudi za kutokuwa na tumaini na kuvunjika moyo ni nini? Alielekeza uso wake upande tofauti. Aliangalia kile ambacho Mungu atakwenda kufanya, japo hangeliona kwa wakati huo. Kwa maneno mengine, aliangalia kwa imani.

Njia ya kushinda ngome za kimihemko za kukata tamaa, kufinyilika, na kutokuwa na tumaini, ni kuangalia katika wakati wote wa shida – sehemu za mapigano, ukame – hadi mwisho. Angalia hadi sehemu yako ya kuyasalimisha mawazo yako, kwa upendo, neema na uaminifu wa Mungu.

Unapofanya hivyo, basi hicho kitu kinachofanya ujihisi jinsi hiyo hakitakumiliki tena. Chochote kinachoenda vibaya maishani hakitakuwa na neno la mwisho. Kumbuka – Shetani anaweza kuwa na “neno”, daktari anaweza kuwa na “neno”, kazi yako, marafiki hata mwenzi wako wanaweza kuwa na “neno”, lakini Mungu ndiye daima analo Neno la mwisho.

Katika Maombolezo 3, Yeremia alikuwa ameshushika moyo. Lakini badala ya kugaagaa humo, alimkumbuka Mungu. Alipoanza kuelekeza mawazo yake kuuelekea wema wa Mungu – licha ya ukweli kwamba hangeliweza kuona wema wa Mungu wakati huo – alianza kujihisi tofauti kuhusu hali ya machafuko aliyokuwamo. Kwa kweli, katika aya ya 18 katika Maombolezo 3, Yeremia anatujulisha kwamba alikuwa amepoteza tumaini lote. Na bado tunaona tumaini lake likirudi mara aliporudisha mawazo yake kwa Mungu. Twasoma:

“Kumbuka mateso yangu, na msiba wangu, pakanga na nyongo. Nafsi yangu ikali ikiyakumbuka hayo. Nayo imeinama ndani yangu. Najikumbusha neno hili, kwa hiyo nina matumaini. Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi, Uaminifu wako ni mkuu. Bwana ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, kwa hiyo nitamtumaini yeye. Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, kwa hiyo nafsi imtafutayo. (Maombolezo 3:19 – 25)

Rafiki, Mungu anaweza kuchukua fujo na kuifanya muujiza ikiwa utaweka tumaini lako kwake. Anaahidi kwamba, “..tena waningojeao hawatatahayarika.” (Isaya 49:23). Kwa kweli, Mungu anaweza kubadilisha mambo yanayokuzunguka kikamili na kukuridhisha kikamilifu, na atafanya mengi zaidi ya kukutoa tu kutoka kwenye utumwa wa kimihemko. Yeye anaweza hata kukusahaulisha jinsi kina chake kilivyokuwa.

Najua kwako kutokuwa na tumaini kunaweza kuonekana kuwa unakulemea, na unaweza hata shangaa jinsi unavyoweza kushinda. Lakini, ikiwa utafanya kama Ibrahimu alivyofanya – yeye aliyetumaini wakati alipokuwa hana lolote… “Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa,” (Warumi 4:18). Mungu ataheshimu imani yako. Anaweza kugeuza maumivu yako ya kihisia kuwa faida ya ushindi.

Tunatumahi kuwa mpango huu ulikuhimiza. Kwa habari zaidi kuhusu wizara, bofya hapa.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Tumaini

Kutokuwa na tumaini ni tauni inayokabili watu wengi wakati moja au mwingine. Hali hii haijahifadhiwa kwa wachache waliochaguliwa. Hata wengi wa mashujaa wetu wa Biblia wanaoheshimika, waliteseka kutokana na kutokuwa na tumaini katika miida fulani fulani. Tony Evans anashiriki mawazo yake jinsi ya kuwa na tumaini, na kushinda hali hiyo ya kukata tamaa katika mpango huu mfupi wa kusoma.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/