Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa YakoMfano

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

SIKU 1 YA 6

Mshipi wa UKweli

“Ndoa ni muungano wa agano uliobuniwa na Mungu ili kuimarisha ustadi na uwezo kwa kila mwenzi kutekeleza kusudi lao katika nyanja za ushawishi ambapo Mungu amewaweka. Kusudi linahusisha kuwa na athari kwa ulimwengu wako kwa wema kupitia kutimiza kusudi lako katika maeneo yote na njia ambazo Mungu amekuweka kufanya hivyo." Tony Evans

Bwana Mpendwa, Umetengeneza kila mmoja wetu kwa utu wa kipekee na ujuzi. Pia umempa kila mmoja wetu matamanio tofauti na shauku ya kipekee katika mambo fulani. Haya yote pamoja na asili zetu tofauti huja pamoja ili kutuelekeza katika mwelekeo wa kusudi letu. Mungu, nisaidie kama mwenzi wa ndoa niwe tegemeo kwa mwenzi wangu katika kutimiza kusudi lao. Nionyeshe kile ninachoweza kufanya ili kuimarisha uwezo wao wa kutekeleza kile ambacho umewaitia kufanya. Najua una kusudi na mimi pia, lakini sitaki hilo liingilie kati na hicho ulichomuumba mwenzi wangu ili atimize.

Kwa kila kusudi huja changamoto, vikwazo, na kukatisha tamaa katika harakati zake. Ninataka kuwa mhakiki kwa mwenzi wangu ili niweze kuzungumza juu ya mambo haya katika mazingira salama, yenye upendo ambapo sijaribu kurekebisha au kuhoji au hata kubadilisha, lakini badala yake nitoe himizo na matumaini ya kuendelea mbele. Nisaidie kuwa baraka katika maisha ya mwenzi wangu ili wafikie utimilifu mkubwa wa kusudi lako katika maisha yao. Niepushe na matamanio ya makuu na hata matamanio ya ubinafsi ambayo yanaweza kuingiia kati ya yale ambayo umetuumba sisi binafsi, na kama wanandoa, kufuata. Katika jina la Kristo, amina.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa Yako

Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia kile kinachoitwa mtazamo na wa mawazo finyu kuhusu ndoa. Kwa hivyo kusudi la kibiblia la ndoa ni nini, na tunapaswa kuombaje kama waumini ili kuhifadhi maana yake? Katika kampeni yetu ya siku sita, Maombi ya Kusudi katika Ndoa Yako, wanandoa wanaweza kuomba kuwepo na maana katika ndoa yao wenyewe, na pia kuthibitisha ufahamu wa kimungu wa muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/