Maombi Ya Kusudi Katika Ndoa YakoMfano
Chapeo Ya Wokovu
“Mungu alimpa Adamu msaidizi anayefaa kwa uhitaji wake wa kutimiza maagizo ambayo Mungu alikuwa ametoa hapo awali, nayo ni kutawala. Mungu hakumpa Adamu Hawa ili tu awe na ushirika fulani. Mungu alimpa Adamu Hawa ili apate mtu wa kushirikiana naye katika kutimiza lengo ambalo alikuwa ameumbwa kwalo. Mungu hakumwumba Hawa kutoka kwa kisichokuwepo ili aweze kuwepo tu. Alimuumba Hawa kutoka kwenye ubavu wa Adamu ili apate mtu wa kushirikiana naye katika kusudi lake la kimungu la kutawala.” Tony Evans
Bwana, kwa kifo cha Kristo, kuzikwa na kufufuka kwake, alitutengenezea kiti pamoja na wewe na yeye katika makao ya mbinguni. Mahali pa mbinguni ndipo ambapo vita vyetu vya kiroho vinafanyika. Asante kwa uwezo ambao tunapewa kupitia wokovu – nguvu sio tu kwa ajili ya umilele bali nguvu za kupigana vita vya kiroho vya ushindi tukiwa duniani. Ulituumba, mwanamume na mwanamke, kwa madhumuni ya kutawala katika eneo na nyanja za ushawishi ulizotuteua kutawala. Kama wanandoa, tunaweza kutekeleza sheria hiyo vizuri zaidi kuliko tungeweza kufanya peke yetu. kwa sababu tuko hapa kuugana mkono na kusaidiana mmoja kwa mwingine.
Utukumbushe sisi ni nani ndani ya Kristo na tumeketi wapi, lakini pia tukumbushe wenzi wetu ni nani katika Kristo na wameketi wapi. Hili litaathiri maneno yetu sisi kwa sisi, heshima yetu mmoja kwa mwingine na shauku na motisha tunayopeana katika kusaidiana kufuata kusudi lao kutoka kwako. Katika jina la Kristo, amina.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Kamwe katika historia ya ulimwengu taasisi ya ndoa haijawahi kuwa chini ya chunguzi kama ilivyo. Kila siku, jamii hutafuta kufafanua upya maana ya kuoa, na Wakristo wanakabiliwa na ukosoaji mkubwa zaidi kwa kushikilia kile kinachoitwa mtazamo na wa mawazo finyu kuhusu ndoa. Kwa hivyo kusudi la kibiblia la ndoa ni nini, na tunapaswa kuombaje kama waumini ili kuhifadhi maana yake? Katika kampeni yetu ya siku sita, Maombi ya Kusudi katika Ndoa Yako, wanandoa wanaweza kuomba kuwepo na maana katika ndoa yao wenyewe, na pia kuthibitisha ufahamu wa kimungu wa muungano wa agano kati ya mwanamume na mwanamke.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://tonyevans.org/