Utukufu Wa Majina Ya MunguMfano
Mwanzo wa Zaburi 8 ni mojawapo ya aya maarufu na inayonukuliwa mara nyingi zaidi katika Maandiko kuhusu fahari ya jina la Mungu:
Ee BWANA, Bwana wetu,
Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote,
Uliyeudhihirisha utukufu wako juu ya mbingu!
- Zaburi 8:1
Majina ya Mungu yanaakisi ukuu na utukufu ulio ndani yake. Jina lake si pungufu ya Ukuu wakeuliotakata. Kugundua na kupata udhihirisho wa majina yake katika maisha yako kutakuingiza moja kwa moja katika uwepo wa Mungu wetu mkuu.
Hivi majuzi mimi na mke wangu Lois tulifunga safari hadi jimbo la Alaska pamoja na washiriki mia kadhaa na wanao unga mkono huduma yetu ya redio, The Urban Alternative – Mbadala Wa Mjini. Alaska ni mojawapo ya maeneo tunayopenda kutembelea, kirahisi ni kwa sababu ya asilia yake yenye kutuliza na mandhari yenye uzuri wa kuvutia. Ila kuna kitu maalum kilichotokea kwenye safari hii. Mwongoza – watalii wetu, ambaye alikuwa amekaribisha na kuongoza zaidi ya safari 90 katika eneo hili hili moja, alituambia hajawahi kuona hali ya hewa nzuri sana kama hii. Kila siku anga ilikuwa safi na nzuri, ikitupa fursa nyingi za kustaajabia fahari ya uumbaji wa Mungu.
Kwa kweli, mambo yalikuwa makamilifu sana hivi kwamba kiongozi wetu wa safari aliita safari hiyo kuwa safari ya watu wasioamini kuwa Mungu yupo. Alisema, "Ikiwa mtu alikuwa si mwamini Mungu alipoingia kwenye safari hii ya baharini, wakati ambapo safari ingelikuwa ikifikia mwisho, hawangeliweza kuwa jinsi hiyo."
Huu ndio aina ya Utukufu ambao Daudi aliandika kuuhusu kwenye Zaburi ya 8. Kama mimi na mke wangu, Daudi alistaajabishwa na uzuri wa uumbaji wa Mungu. Alijibu kwa kutambua udogo wake mwenyewe na udogo wake kwa kulinganisha na ukuu wa jina la Mungu lililoonyeshwa kupitia uumbaji:
Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,
Mwezi na nyota ulizozifanya;
Mwanadamu ni nini hata umwangalie,
Na mwanadamu hata umwangalie?
Zaburi 8:3 – 4
Kumbuka, hutapata kuona uwezo wa nguvu ya majina yake katika maisha yako ikiwa una hisia yenye kiburi kuhusu thamani yako mwenyewe.
Ukuu wa Mungu umetengwa kwa ajili ya wale wanaojua vya kutosha kujua kwamba hawajui lolote hata kidogo. Kwa maneno mengine, huwezi kujua fahari ya majina ya Mungu mpaka upate kufikia na kufahamu sana udogo wako mwenyewe.
Kuhusu Mpango huu
Mungu ana majina kadha wa kadha ambayo yanamwelezea katika Maandiko. Kila jina hutuambia sifa na moyo wake kwa njia ya kina na kibinafsi. Katika mpango huu wa kusoma na Tonay Evans, fichua ukuu wa majina ya Mungu.
More
Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative