Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Utukufu Wa Majina Ya MunguMfano

Utukufu Wa Majina Ya Mungu

SIKU 4 YA 4

Maneno ya Yesu mwanzoni mwa Sala ya Bwana yanazungumzia pia ukuu wa jina la Mungu:

Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe.
– Mathayo 6:9

Neno kutukuzwe linatokana na neno la Kigiriki ambalo kwa kawaida tunatafsiri kama takatifu. Kwa maneno mengine, hii ina maana kwamba majina ya Mungu ni ya kipekee. Siyo kwetu sisi kuyachanganya na jina la mtu mwingine yeyote au kulichukulia kwa wepesi. Majina ya Mungu yametukuzwa. Yanapaswa kuheshimiwa, kupewa taadhima, na kutendewa kwa heshima inayostahili.

Kwa mfano, ikiwa rais wa Marekani angeingia kwenye chumba hiki, huwezi kuzungumza naye kwa njia isiyo rasmi. Huwezi kusema, "Kuna nini, Rafiki?" Wadhifa ya rais inadai kiwango fulani cha kutambuliwa na kuheshimiwa.

Kwa wazi, majina ya Mungu yanapaswa kuheshimiwa hata zaidi kuliko vile tungempa heshima mtu yeyote duniani. Tumeagizwa kuyatakasa majina yake—sio tu kwa kuyatamka majina yake bali jinsi tunavyofikiri na kuyatafakari pia

Kutukuza majina ya Mungu kunamaanisha kuyatendea kana kwamba yana uzito—kana kwamba ni ya maana sana. Inamaanisha tunatambua kwamba Mungu si wa kawaida na kwamba majina yake si majina yake si ya kawaida. Sisi si hatufanyi mazaha juu ya majina yale. Hakika hatupaswi kutaja majina yake bure. Lakini tunaweza pia kutukuza majina ya Mungu kwa kuchagua tu kuyatumia kwa njia inayowasilisha kicho, heshima, ibada, na hata hofu.

Kujua majina ya Mungu ni kupata uzoefu wa asili yake, na kiwango hicho cha uhusiano wa dhati kimehifadhiwa kwa wale wanaomtegemea kwa unyenyekevu. Kwa sababu Mungu hatashiriki utukufu wake na mwingine (Taz Isa. 42:8), ni lazima tunyenyekee ikiwa kwa kweli tunataka kumjua. Ni lazima tutambue udogo wetu kabla ya kupata umuhimu unaokuja kwa njia ya yeye pekee.

Jina la Mungu ni tukufu. Ni la kipekee na limetengwa—kitu kinachostahili kutakuzwa kupitia matendo na mitazamo yetu. Ni pale tu tunapolitakasa jina la Mungu ndipo tunaweza kutumaini kupata nguvu zake kikweli.

Tunatumai kuwa mpango huu umekuhimiza. Ili ujue zaid kuhusu huduma ya Tony Evans, bofya hapa.

siku 3

Kuhusu Mpango huu

Utukufu Wa Majina Ya Mungu

Mungu ana majina kadha wa kadha ambayo yanamwelezea katika Maandiko. Kila jina hutuambia sifa na moyo wake kwa njia ya kina na kibinafsi. Katika mpango huu wa kusoma na Tonay Evans, fichua ukuu wa majina ya Mungu.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative