Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Acha! Usiwe Na Wasiwasi ZaidiMfano

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

SIKU 1 YA 7

Usiwe na wasiwasi!

Kuna mapambano maishani ambayo yanaweza kuwa ngome za kihisia - mambo ambayo yanakukamata mateka na kukuzuia kumtumikia na kumwamini Mungu kwa moyo wako wote na kuwa na maisha tele ambayo ameahidi. Mojawapo ya ngome zinazoharibu zaidi ni wasiwasi. Wasiwasi inapatikana katika kila umri na ni kikwazo cha kuendelea mbele.Inapokuwa ngome katika maisha yako, basi infanyika kuwa mwenendo wa maisha yako.

Tunakuwa na wasiwasi kuhusu mambo mengi - watu wanafikiri nini kutuhusu, je, tunaonekana kuwa tunafaa, je, tuna afya njema, na je, tuna pesa za kutosha. Ikiwa una mwelekeo wa kuwa na wasiwasi, hakuna kikomo kwa uwezekano wa kuwa na wasiwasi.

Watu hukabiliana na wasiwasi kwa njia kadhaa - wengine hunywa mvinyo ili kuipuuza, wengine hununua vitu vya kukengeusha, wengine hulala usingizi au kulala mapema ili kuiepuka. Hakuna hata moja ya tiba hizi inafanya kazi kwa sababu hofu bado inaendelea kuwepo. Katika Mathayo 6:25, 31 – 34, Yesu alisema mara tatu, "Msisumbuke!" Neno la Kigiriki linalotumiwa kwa “wasiwasi” ni dhana ya kunyongwa au kusongwa. Wasiwasi inakuacha ukiwa umechanganyikiwa unapopaswa kuwa huru, na kama wewe ni mfuasi wake, basi unapaswa kuizuia.

Wasiwasi ni dhambi kwa sababu ni mashaka katika uwezo na wema wa Mungu. Baadhi ya watu hawapendi kuiita wasiwasi kuwa ni dhambi – wao huwa “wanajishughulisha” tu kuhusu jambo fulani. Unatofautishaje kujishughulisha na wasiwasi? Kujishughulisha kihalali ni wakati unapodhibiti mawazo na hisia zako na wasiwasi ambayo si halali, ni wakati jambo linadhibiti mawazo yako, vitendo na hisia zako.

Yesu alisema, “Kwa sababu hiyo nawaambia, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mtakunywa nini, wala miili yenu, mvae nini. Je, maisha si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani, na bado Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Je, ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?” (Mathayo 6: 25 – 26) Sababu ya sisi kuwa na wasiwasi ni kwamba tunazingatia mamlaka isiyo sahihi. Ikiwa Baba yetu anawalisha ndege ambao hawana nafsi, je, hatatutunza hata zaidi kwa kuwa sisi ni wa thamani zaidi kwake? Kumbuka ahadi yake kwamba hatakuacha wala hatakutupa, kama kiuasumu cha kwanza ya dhidi ya kuwa na wasiwasi.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

Mipango inayo husiana