Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Acha! Usiwe Na Wasiwasi ZaidiMfano

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

SIKU 4 YA 7

Wivi wa Utambulisho

Marekani kwa sasa ina tatizo la wizi wa utambulisho. Maendeleo ya teknolojia na kuhamia kwetu kwa kununua na kuuza bidhaa mtandaoni kumeongeza mzozo huu. Watu wanaoiba vitambulisho vya wengine watatumia pointi zao za mkopo na akaunti za benki kuishi maisha ambayo kwa kweli hayawaakisi wao wenyewe, bali ya mtu mwingine.

Jambo kama hilo hutokea tunapohangaikia sana maoni ya watu wengine badala ya yale ambayo Mungu anafikiri. Tunaanza kuchukua utambulisho wa watu tunaowaona kwenye televisheni au watu waliofanikiwa tunaowasoma kwenye magazeti badala ya kusalia kuwa wakweli kwa jinsi tulivyo. Kuhangaika ikiwa twakubalika na watu wengine ni mojawapo ya ngome kuu kushinda. Hii ni tofauti na utegemezi mwenza ambao tuliangalia hapo awali. Ngome za kuwafurahisha watu zaweza kuwa sababisho ya ngome nyinginezo kama vile kutafuta kuwa mkamilifu kwa kila utendalo, kufanya kazi kupita kiasi, kushikwa na tamaa sana ya mawazo ya kutaka kubadili mwonekano wa mwili, na matendo.

Sababisho ya ngome hii ni nini? Katika Wagalatia 1, tunasoma kuhusu viongozi wa kidini walioitwa Wayahudi ambao walitaka kuwapima Wakristo kwa kutumia kiwango cha utendaji "chini ya sheria" na hivyo kuacha neema.

Katika Wagalatia 1:10, Paulo anena kuhusu hawa vioingozi waliokuwa wakiwatakia mema, waliokuwa wakinukuu maandiko, nao pia walikuwa wakiwapasua watakatifu kutoka kwenye neema, “Je, sasa ninatafuta upendeleo wa wanadamu au wa Mungu? Au je, ninajitahidi kuwapendeza wanadamu? Kama ningeendelea kuwapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.” Paulo anasema kwamba inawezekana kuwa na mwelekeo kwa watu zaidi kuliko kuwa na mwelekeo kwa Mungu. Mithali 29:25 inasema, “Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; bali yeye amtumainiye BWANA atatukuzwa.”

Shetani hutumia hitaji letu halali la kukubaliwa kwa njia isiyo halali ambayo inaweza kutufanya tuishi chini ya utambulisho wa uwongo. Utaona jinsi watu walivyochanganyikiwa, wanaotaka kufurahisha kila mtu – dakika moja wanampendeza mtu mmoja, dakika inayofuata wanamfurahisha mtu mwingine. Wanapaswa kuwa karibu na watu wanaowafanya wajisikie vizuri - la sivyo wanakuwa wenye huzuni.

Utaanza kushinda ngome yako ya wasiwasi wakati unapoamua kwamba kile ambacho Mungu anasema juu yako ndicho chenye umuhimu zaidi.

Mungu asiyebadilika anakupenda kwa upendo wa milele. Ameona kilio chako chenye uchungu, siku zako bila mapambo au nywele ambazo hazijachanika, na amesikia kelele zako zenye hasira na kelele zenye majivuno…. bado yeye anakupenda! Ikiwa unaendeshwa na kibali cha watu kumbuka kuwa wao wanaweza kukosea, na hisia zao zinabadilika.

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi

Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.

More

Tungependa kuwashukuru The Urban Alternative (Tony Evans) kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: Home - The Urban Alternative

Mipango inayo husiana