Soma Biblia Kila Siku/ FEBRUARI 2023Mfano
Mungu anaweza kuruhusu machafuko ili kutufundisha na kututiisha. Pia huzuia vita ili kubaki kuwa na amani. Leo tunaona jinsi Rehoboamu alivyojiandaa kwenda kupigana kwa ajili ya taifa la Israeli, lakini Mungu anamtuma Shemaya kumzuia Yeroboamu asianzishe vita, kwa kuwa mgawanyiko uliotokea una kibali mbele za Mungu. Bwana akasema, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Na watu wa Yesu walikubali kumsikiliza Mungu kuliko mfalme: Basi, wakalisikiliza neno la Bwana, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la Bwana (m.24). Je ni mara ngapi Mungu amesema na wewe, ukaisikia sauti yake na kuitii?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Februari 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Warumi na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/