Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Bwana Yesu aja (3:13, Wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote)! Hivyo tuwe tayari ili tumlaki Bwana (4:17). Kuja kwake hugawa watu wote katika makundi mawili: 1. Wasioamini ni wa usiku, wamelala usingizi wa kiroho gizani. Hawamngoji Yesu, kwa hiyo kwao kuja kwake ni kama ajavyo mwizi. Hakika hawataokolewa (m.3). 2. Waumini ni wa mchana, hutoa nuru kwa imani na upendo wao. "Kuwa na kiasi" ni "kutokulewa" kama wasioamini. Ni "kuacha lolote lile litugeuzalo tulitazamie hilo badala ya Yesu". Tukikesha hivyo tumaini litatulinda kama chapeo mpaka Yesu aje (m.8, Sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu). Hakika tutaokolewa!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/