Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Wasiomwamini Yesu hakika hawataokolewa (5:3). Lakini si mpango wa Mungu kwao. Hakuwateua kwa ajili ya upotevu wa milele. Maana Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu (m.9) na kupata kujua yaliyo kweli (1 Tim 2:4). Twaweza kuwa na uhakika, maana Yesu alikufa kwa ajili yetu (m.10; ling. swali katika Rum 8:32, Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaji kutukirimia na mambo yote pamoja naye?). Katika m.10 Paulo anabadilisha mfano. Hapo maana ya kulala (m.10) si kulala usingizi wa kiroho kama katika 5:6-7, bali kulala mauti (4:15). Yaani tuwe hai, tuwe tumekufa, Yesu akija, sote tutaishi pamoja naye milele. Tujengane katika tumaini hili!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/