Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

SIKU 5 YA 31

Somo hili huthibitisha kwamba imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi (Mdo 14:22). Ni kwa sababu kama wasioamini walivyomwudhi Yesu, wanawaudhi pia wamfuatao (m.14-15, Ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi; ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi). Lakini sasa Injili ni Neno la Mungu (m.13, Mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli). Kwa hiyo huwapa waumini kushinda dhiki hizo wapate kuokoka, bali wapinzani wake watapatwa na hasira ya Mungu (m.16, Hasira imewafikia hata mwisho) pamoja na ghadhabu itakayokuja. Maana Yesu peke yake ndiye mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja (1:10). Kazi yote ya Paulo hulenga kuja kwa Bwana wake Yesu (m.19, Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?). Furaha ya Paulo ni kumletea Yesu waumini wengi wanaomsifu. Je, ni furaha yako pia, ukifanya kazi ya Mungu?

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023

Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana