Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023Mfano
Paulo alijisikia kama mfiwa msibani, wakati hakujua habari ya Wathesalonike (m.7, Ndugu, tulifarijiwa kwa habari zenu, katika msiba na dhiki yetu yote, kwa imani yenu). Kwa hiyo faraja ya Paulo ni kubwa, akisikia wanadumu katika imani. Angalia Paulo anavyomtegemea Mungu katika yote: Kama vile, wakati Paulo hakujua hali yao, mahangaiko yake yalivyomfanya awaombee, sasa habari zao njema zinamfanya amshukuru Mungu kwa ajili yao. Mungu apewe sifa zote! Maana ni neno lake peke yake lililowahifadhi, ingawa pia Paulo alijibidisha kwa ajili yao. Mapungufu ya imani yao (m.10, Usiku na mchana tunaomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu, na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu) yalitokana tu na muda mfupi aliokaa nao (majuma 3).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/