Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Musa alimrudia mkwewe, akatwaa familia yake akaenda Misri. Mungu alimwambia mapema juu ya ukaidi wa Farao, mapigo na hata kifo cha mzaliwa wa kwanza ambavyo ukaidi huo utawasababishia Wamisri. Njiani Mungu alikutana na Musa ili kumkumbusha wajibu wake wa kumwingiza mtoto wake katika agano (Mwa 17:10). Mkewe alimtahiri mtoto wao ili kuokoa maisha ya Musa. Haruni alikuwa tayari kuongea maneno ya Mungu, na Waebrania walipoona zile ishara na kusikia kuwa Mungu ameyaona mateso yao waliamini na kuabudu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/