Soma Biblia Kila Siku/ Aprili 2023Mfano
Mkutano wa kwanza wa Musa na Farao ulilenga kuwaombea kibali Waebrania waruhusiwe kwa siku tatu kwenda kuadhimisha sikukuu jangwani. Farao hakumcha Mungu na kuuliza kwa kejeli, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake? (m.2). Kwa kiburi hakutoa kibali cha kuwapeleka watu wa Mungu jangwani ili wamtolee Bwana sadaka. Badala yake aliwalaumu kuwa ni wavivu na akawawaongezea kazi kubwa zaidi. Ingawa mkutano huu ulionekana wa hasara kwa Waebrania, tendo la Mungu kuwaokoa liliendelea alivyopanga.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku/Aprili 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Yohana, Mithali na Kutoka. Karibu kujiunga na mpango huu bure
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/