Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 17 YA 30

Umpokee Onesimokama mimi mwenyewe.Mimi nitalipa deni lake. Hivyo Paulo ni mfano wa Yesu anavyowaombea waamini kwa Baba. Katika 1 Kor 7:22 Paulo anasema,Aliyeitwa katika Bwana hali ya utumwa, ni huru wa Bwana. Vivyo hivyo yeye naye aliyeitwa hali ya uhuru, ni mtumwa wa Kristo. Tunaona jinsi neno hili linatimia katika maisha ya Onesimo na Filemoni. Onesimo aliye mtumwa, nihuruwa Bwana, maana analipiwa deni lake na kuachwa huru kwa kuombewa na Paulo. Filemoni aliye huru, nimtumwawa Bwana, maana Yesu ameokoa nafsi yake kwa mahubiri ya Paulo. Ni maana ya analoandika Paulo katika m.19,Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako. Inaonekana wazi zaidi katika tafsiri ya Biblia Habari Njema inayosema,Sina haja ya kusema kwamba wewe unalo deni kwangu la nafsi yako.Hali hiyo ya Filemoni inamfanya kumwacha huru Onesimo. Linganisha na Mt 6:12 tunaposoma,Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/