Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano
Tujihadhari na uovu wa Ahabu, na vilevile na yale madogomadogo yawezayo kutuangusha! Yehoshafati alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana isipokuwa katika mambo mawili:Mahali pa juu[palipofanyika ibada ambazo hazikuwa sahihi]hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa dhabihu wakafukiza uvumba katika mahali pa juu(m.43), naakafanya amani na mfalme wa Israeli(m.44). Tutambue kuwa uovu maishani mwa Ahabu upo pia mioyoni mwetu. Tusifanye amani nao! Bali tuishi nuruni ili tusafishwe! Kama ilivyoandikwa katika 1 Yoh 1:7,Tukienenda nuruni, kama yeye[Mungu]alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. Zingatia hiyo, kisha omba: Bwana Mungu, nakuomba unipe moyo unaonyenyekea na kuungama makosa ninayoyatenda. Unisamehe, na unishike mkononi mwako nisipotee bali nikuishie wewe maisha yangu yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/