Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

SIKU 23 YA 30

Wakati ule Mataifa waliamini kwamba kila taifa lina mungu wake, na walitambua Mungu wa Waisraeli kama mungu wa milima. Lakini Waisraeli walishinda vita hata katika nchi tambarare. Sababu siyo kwamba walimwamini sana Mungu, bali yeye alitaka kujidhihirisha kwa wote kama Mungu wa kweli duniani pote. Ndiyo maana nabii anapomwambia Mfalme wa Israeli, Bwana asema hivi, Kwa sababu Washami wamesema, Bwana ni Mungu wa milima wala si Mungu wa nchi tambarare; basi nitawatia makutano haya yote walio wengi mkononi mwako, nanyi mtajua ya kuwa ndimi Bwana(m.28). Ahabu hakutii maagizo ya Mungu alipomwacha mfalme Ben-hadadi kuishi na hata kupatana naye. Kwa sababu agizo la Mungu lilikuwa hivi,Utawapiga; wakati huo ndipo uwaondoe kabisa; usifanye agano nao, wala kuwahurumia; wala usioane nao(Kum 7:2). Sisi je, tunafanana na Ahabu aliyeamua mwenyewe kama alivyoona ni vema?

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Juni 2023

Soma Biblia Kila Siku Juni 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Filemoni na 1 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana