Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 28 YA 31

Mungu ni wa milele. Umilele wake unatokana na ukweli kuwa yeye alikuwako, yupo na atakuwepo (Kut 3:14). Kwa sababu ya ujinga wake, mtu hajui ukuu na mamlaka ya Mungu, kama asipotafuta kuelimishwa na neno la Mungu lililo la kuaminika. Angalia kwamba Aguri anauliza jina la mwana wa Mungu ni nani:Jina la mwanawe, kama wajua?(m.4c). Tunaweza kumfahamu Mungu kwa njia ya Kristo, Mwana wa Mungu. Pia ni kwa njia yake tu, tunafahamu jinsi ulimwengu ulivyoumbwa, maana Kristo alishiriki katika uumbaji wa Mungu.Naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye(Kol 1:15-17).

Andiko

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana