Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 1 YA 31

Mateso ya mgonjwa tuliyesoma habari zake tunaweza kuyaelewa japo kidogo tukizingatia muda aliougua – miaka 38! Mfumo wa tiba na taratibu za kijamii na kidini havikumsaidia. Kibaya zaidi, hata hakuna aliyemtambua kwamba na yeye alikuwapo. Katika kulalama kwake anasema hana mtu wa kumtia birikani. Yesu akamwona, kwa huruma akamponya ugonjwa wake. Baadaye akamwonya pia asitende dhambi tena. Fikiri maisha yako. Ni wapi umeugua na kushindwa? Umtegee Yesu sikio lako, ndiye jibu lako.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana