Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Wayahudi walitaka kumwua Yesu.Hata nduguze hawakumwamini(m.5) wala kumpenda. Maana walimpa Yesu ushauri ambao walijua utampambanisha na Wayahudi. Swali muhimu la kujiuliza ni, “Kwa nini hao walimchukia Yesu?” Katika m.7 Yesu anasema:Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi; bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu. Kwa hiyo watu wa ulimwengu huu humchukia Bwana Yesu kwa sababu anawaambia ukweli. Mimi na wewe tunapokeaje ushuhuda wake juu yetu? Tukiupokea tutachukiwa na watu wa ulimwengu huu kwa sababu wanamchukia Yesu. Lakini tuhesabu tuna heri, maana neno lake ni kweli. Tulinganishe na anachosema katika Mt 5:11-12:Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/