Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 14 YA 31

Je, wewe unamfahamu Yesu kuwa nani? Ni jambo muhimu sana, maana ni hatua kuelekea kumwamini Yesu. Hapo haitoshi kuwa na elimu kubwa ya dini, maana tunaona viongozi wa kiyahudi hawakumfahamu Yesu kuwa yu nani. Jambo muhimu zaidi ni kusikiliza ushuhuda wa Yesu, maana huu unatusaidia kumwamini, kama ilivyoandikwa kuhusu waliomsikiliza siku ile: Yesualipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini(m.30). Zingatia Yesu anavyojitambulisha katika m.12, 19 na 23:Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. ...Mimi hamnijui, wala Baba yangu hammjui...Mimi ni wa juu; ninyi ni wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.Yaani Yesu anasema si mzawa wa Yusufu, bali ni Mwana wa Mungu. Ni juu ya ulimwengu kama Mwokozi wake. Tunapomwamini hatutakufa katika dhambi zetu!

siku 13siku 15

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana