Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Tumezoea kusema Yesu anaweza yote. Lakini leo Yesu anatuambia jambo ambalo hawezi. Unajua ni nini hilo? Katika m.19 imeandikwa,Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile. Yesu hakupunguza wala kuongeza wala kubadilisha lolote aliloliona kwa Baba yake anayempenda. Kwa hiyo amemfunua Mungu kikamilifu kwetu. Katika m. 24-25 Yesu anasisitiza akisema,Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani. Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai. Tusipomwamini Yesu tu wafu kwa Mungu. Lakini sauti ya Yesu inatuhuisha tukiyapokea maneno yake kwa imani. Tunapewa uhusiano mwema na Mungu. Ndio uzima usiokoma. Hata kifo cha kimwili hakiwezi kuukomesha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/