Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano
Mahitaji ya mtu kimwili na kiroho ni nini? Uponyaji ulivuta watu wengi kumwendea Yesu.Mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa(m.2). Ishara ya kuwalisha watu zaidi ya elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili, kisha kubaki vikapu 12, iliwafanya watu wamwone kuwa nabii, na wakasema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni(m.14). Lakini je, lengo la ishara ni hili tu? Kwamba watu wale na kusaza tu na wamwone Yesu kuwa nabii tu? Hasha! Ishara zitusaidie kumwamini Yesu kuwa ndiye Kristo, Mwana wa Mungu na Mwokozi wetu. Kumbukakuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake(Yn 20:30-31). Utoshelevu wa mahitaji ya mtu ni uzima wa milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/