Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

SIKU 5 YA 31

Walipotaka kumfanya awe mfalme, Yesu hakutaka, basi akawatoroka,akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake(m.15). Bwana Yesu alikataa milki za ulimwengu na fahari zake zote. Kwa nini alikataa? Jibu la swali hili ni kama anavyoeleza akisema,Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa(Yn 18:36).Ishara za kutembea juu ya maji bila kuzama na kushinda tatizo la umbali zinaonyesha Yesu yu mkuu sana, na yuko juu zaidi ya kanuni za asili na maumbile za dunia hii. Hakika Yesu ni Bwana, na ufalme wake sio wa ulimwengu huu! Sote tumpokee maishani mwetu kama wanafunzi walivyompokea chomboni.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku/AGOSTI 2023

Soma Biblia Kila Siku Agosti 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kuelewa somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu Yohana na Mithali. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

Mipango inayo husiana