Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

SIKU 2 YA 30

Waisraeli walimhesabu Paulo kama adui wao, maana alitetea kuwa watu wa Mataifa wataweza kuwa watoto wa Mungu kwa kumwamini Kristo bila kutahiriwa na kufanywa Waisraeli. Hivyo alihitaji kuwashuhudia upendo wake kwa Waisraeli (m.1-5). Na leo hujitetea kutokana na neno la Mungu:Si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao(m.8). Linganisha na Gal 3:26-29 inayosema:Ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. Tangu awali Mwisraeli wa kweli ni yule wa ahadi. Esau hakuwa mtoto wa Mungu ingawa ni wa ukoo wa Ibrahimu!

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/