Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023Mfano
Baada ya kila fundisho Paulo anauliza swali la udadisi ambalo anajua Wayahudi wangeuliza. Anayoelezea leo yanapita ufahamu wa binadamu:Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwani kuniumba hivi(m.20)?Kwa hiyo Paulo hatafuti kuiridhisha akili ya binadamu kwa kila jambo. La muhimu zaidi kwake ni kuonyesha msingi wa kila fundisho katika Maandiko Matakatifu, maana ni kweli. Zingatia ukuu wa Mungu. Anasema,Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye(m.15). Tenamaandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote(m.17).Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu(m.16). Fundisho: Kuokoka kunategemea neema ya Mungu tu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/